Sababu Za Kushindwa Kwenye Biashara Za Mtandao

 

 

 

Mimi binafsi nilianza biashara za kwenye mtandao (Internet Marketing) mwishoni mwa mwaka 2012. Nilijiunga na makampuni kadhaa ya Marekani, Canada na Uingereza na aina ya biashara niliyofanya wakati huo ilikuwa zaidi ni Affiliate Marketing. Wale ambao wapo SFI (Strong Future International) – nafahamu watanzania, waganda, wanyarwanda na wakenya wengi ni wanachamama wa SFI – wanafahamu maana ya affiliate marketing. Kampuni nyingine ni Worm Vegas (Word of Mouth Convention) na ParadoxCash. Nilifanikiwa kuanza kupata pesa kiasi na kujifunza mambo mengi sana ya ujenzi wa tovuti, search engine optimization, webpage creation, social media marketing na mengineyo. Lazima nikiri kuwa nilipata mengi sana na kwamba wenzetu wapo mbali sana. Moja ya tovuti zangu iliyopata umaarufu sana ni Home Based Business Training (2014).

Nilianza biashara hapa Tanzania mwishoni mwa mwaka 2014, nilibadilika na kufanya Network Marketing kwa sababu ndiyo iliyopo hapa kwetu na bado naendelea na biashara hiyo hadi sasa.

Kuna baadhi ya watanzania wachache wameachana kabisa na umaskini kwa kufanya biashara hii ya mtandao wakati wengi bado wanahangaika sana. Nchin Afrika ya Kusini, watu walioachana na umaskini ni wengi zaidi na huko Nigeria kuna mabilionea waliotokana na biashara hii. Nilipata wazo la kuchunguza ni kwa nini watu wengi hapa kwetu wanashindwa kupata mafanikio kwenye biashara hii, ndipo nilipoisoma mada moja iliyoandikwa na ndugu Beverly Nadler – The Reasons People Don’t Succeed. Mada hii ilinigusa sana kwa sababu niliona inalifafanua tatizo la huku kwetu kwa asilimia 100 na nikaamua kuitafsiri ili wapenda maendeleo wengine wote waweze kunufaika nayo. Nasema wapenda maendeleo wote, kwa sababu yaliyoandikwa hapa yanahusu biashara nyingine ya aina yo yote. Kimsingi, nimechukua vichwa vya habari kama alivyoviandika lakini katika ufafanuzi mara nyingine nimeingiza mawazo yangu kama mimi binafsi nilivyoona hali inavyokwenda hapa Tanzania.

Kwa Nini Watu Wanashindwa?

Ndugu Nadler alianza kwa kuelezea baadhi ya sababu za watu kushindwa kwenye biashara za mtandao lakini akatoa tahadhali kuwa pamoja na kwamba inabidi kuwa mwangalifu na sababu hizi, bado hizi si sababu kuu. Sababu hizi zinachochangia tatizo kwa maoni yake ni:

Kutotumia Vizuri Nyenzo Za Kampuni

Watu wanashindwa kupata mafanikio kwa sababu ya kutotumia nyenzo zinazotolewa na kampuni. Makampuni mengi sasa hivi (tofauti na miaka ya nyuma), yanatoa nyenzo nyingi za kazi, wakati wa kukiunga na kampuni na baada ya kujiunga. Vinaweza kuwa vipeperushi, CD, vitabu na hata software. Watu wengi huvifungia ndani vitu hivi bila ya kuvitumia hata siku moja.
Katika moja ya kampuni niliyojiunga, nilistaajabu kuona hata upline member wangu hajui compensation plan ya kampuni yetu. Si hili tu, hakujua hata kama kuna ppts nyingi zilizotolewa kwa ajili ya mafunzo.
Kama hujui compensation plan ya kampuni yako, unachokifanya ni nini? Kampuni zote za mtandao zina njia nyingi za kupatia pesa, ikiwa huijui compenstion plan, umelengaje kupata pesa katika kampuni unayofanya nayo kazi?
Unapomweleza mtu kuhusu fursa ya kampuni yako, mtu hukupima uelewa wako na jinsi unavyokiamini unachokisema. Kumbuka kuwa watu wengine unaowapa fursa wamekwisha fanya kazi na kampuni nyingine. Unatoaje presentation ya kampuni yako ukaeleweka kama huna ppt au nyenzo nyingine inayoeleweka?
Kwa hili mimi nakubaliana kabisa na mwandishi wa ile mada. Sababu ya msingi hapa ni kwamba, msingi wa biashara ya mtandao yo yote ni duplication, yaani mwenyeji kumfundisha mgeni kile anachokifahamu, na hivyo hivyo zoezi hilo kuendelea kizazi hadi kizazi.
Kama tunahitaji kufanikiwa, inatubidi kubadilika na kuwa wasomaji na wapekuzi wa kujua undani wa biashara tunazozifanya.

Kuhamahama

Watu wengine wameshanaswa kwenye ugojwa wa “kuvizia mpya”, wakisikia fursa mpya tu, wanakuwa wa kwanza kwenda kujiunga. Hakuna kazi wanayoweza kufanya kwa sababu mpya ni nyingi na zitaendelea kutoka.
Ushauri kwa kundi hili ni kukaa chini na kutafakari kuhusu wanachofonya, kwa sababu bila kificho, kundi hili la watu kamwe halitakuja kuona mafanikio kwenye biashara hizi.

Kukosa Muda wa Kutosha

Kuna watu wanaopenda kufanya biashara za mtandao lakini wana biashara nyingine, ajira au shughuli nyingine zinazowabana na kukosa muda wa kuzihudumia biashara zao za mtandao. Hapa kwa kweli sio kosa lao. Labda moja ya ushauri wa kuwapa ni kuwa na mtu atakayefanya kazi kwa niaba yao na kuomba msaada kutoka kwa upline member.

Kutochagua Vizuri Kampuni

Kuna vigezo vingi ambavyo mtu anatakiwa avitazame kabla ya kujiunga na kampuni ya mtandao. Kwanza ni kujua historia ya mmiliki wa kampuni na ya kampuni yenyewe. ukijiunga na kampuni ambayo imeanza na kufa wewe ukiwemo ndani yake, maoni yako yatakuwa, biashara za mtandao ni za kitapeli, wakati biashara kuanza na kushindwa ni kitu cha kawaida. Wengi hujiunga tu bila kufanya uchunguzi.

Watu wengine wanashindwa kwa sababu wanajiunga na biashra ambazo haziwafai. Mfano mzuri ni pale mtu anapojiunga na kampuni ambayo bidhaa zake yeye mwenyewe binafsi hazipendi.

Kuna watu ambao biashara za mtandao haziwafai kabisa. Kuwauzia watu wengine bidhaa ni kitu ambacho hakipo kabisa ndani ya damu yao. si kituu cha ajabu kwa sababu si kila kitu kitamfaa kila mtu.

Mwandishi, Beverly Nadler, anaamini na kuandika kuwa sababu hizi SIYO SABABU KUU za watu kushindwa katika biashara za mtandao. Yeye anamini kuwa sababu kubwa ni kuwa na mtazamo chanya, mazoea tofauti na mpangilio wa akili ulio tofauti na mambo ya biashara. Kwa lugha yake mwenyewe;

The real reason most people fail is because they have the wrong “mind-set”, conditioning and programming.

Anaamini kuwa kuna pengo la kuzibwa katika mafunzo wanayopewa wanachama wapya wanapojiunga na makampuni ya biashara za mtadao. Watu wengi hujiunga wakiwa au wakitokea kwenye ajira ambako mtizamo wao ni wa kuajiriwa – job or employee “mind-set. Hawajafunzwa kuwa na fikra au kuwa na tabia za mfanyabiashra kibiashara. Inatakiwa watu haw wapikwe (kupewa mafunzo ya kisaikolojia) ili waweze kuwa na akili ya kibiashara.

Kifupi, inapasa watu hawa kufundishwa ili kwa utashi wao:

1. Waweze kujiamini na kuanza kuona kuwa wana uwezo wa kufanya biashara
2. Waiamini biashara ya mtandao,na kutokwa na mawazo ya kuwa si biashara halali
3. Waiamini kampuni wanayojiunga nayo na ubora wa bidhaa/huduma zinazotolewa.

Usisite kutoa maoni yakoau kuuliza maswali kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kuona kuwa tumekujibu na kwa wakati mwafaka.
Laurian.

 

 

 

Comments are closed.