KAMPUNI YA GREEN WORLD YAANZA SEMINA ZA MWEZI MMOJA

 

Mafunzo ya budiman septemba 7, 2016

 

Pamoja na kuwa kampuni ya Green World inatoa nyezo nyingi za aina tofauti ili kuwawezesha wanachama wake kufanya kazi kwa ufanisi, haijasahau kuhakikisha kuwa mafunzo ya kina yanatolewa kwa wanachama wake. Kuna mafunzo yanayotolewa mara kwa mara katika ofisi za kampuni hiyo, na mara chache, analetwa mkufunzi wa nje ili wanachama wake wapate uzoefu wa nchi nyingine katika kuifanya biashara ya kampuni hiyo.

Kuanzia leo tarehe 7 Septemba 2016, mkufunzi mkuu wa kampuni mwenye makao yake makuu kwenye mji wa Ontario Canada, ndugu Budiman, ameanza mafunzo katika ofisi ya kampuni hiyo iliyoko eneo la Upanga, makabala na makao makuu ya JWTZ. Mafunzo haya yatafululiza kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja. Mafunzo yatatolewa kwa wanachama wapya, na kuna mafunzo ya viongozi – wale ambao tayari wamekuwepo ndani ya kampuni hiyo kwa kipindi kirefu na waliofikia ngazi za juu. Lengo ni kuhakikisha kuwa wanachama wote wanaijua vizuri biashara ya kampuni hiyo na kuwawezesha kuifanya kwa ufanisi zaidi.

Mafunzo yataendelea katika ofisi ya kampuni hii kila siku nne za kwanza za wiki, yaani, jumatatu hadi alhamisi.

Katika kuhakikisha kuwa wanachama walio nje ya Dar Es Salaam nao wanapata mafunzo hayo, mkufunzi huyu ataelekea katika miji ya Dodoma, Mwanza, Mbeya na Arusha. Ratiba ya nje ya Dar Es Salaam kwa sasa hivi ni kama ifuatavyo:

 

Dodoma – 10/9/2016
Mwanza – 17/9/2016 – Gold Crest Hotel
Mbeya  - 24/9/2016
Arusha – 1/10/2016

 

Kama wewe ni mtu unayependa kuona kuwa umetimiza ndoto zako za kufikia maisha ya uhuru, usikose kuhudhuria semina hizi za mmoja wa wakufunzi wanaoheshimika katika dunia hii. Gharama za kuhudhuria semina hizi ambazo zina thamani ya dola nyingi ni BURE – kwa hisani ya ndugu Budiman.

Wanachama hai wa kampuni ya Green World wanakumbushwa kuwa hakuna nafasi ya kuilinganisha na hii katika kujenga jumuia zao za wafanya biashara wa Green World. Wanaombwa kuhakikisha kuwa wanawapa taarifa watu wengi kadri watakavyoweza.

 

Laurian.

Comments are closed.