Bidhaa Za Kulinda Afya Za Green World
Utangulizi
Kadiri siku zinavyokwenda, maendeleo ya binadamu yanazidi kuongeza kasi; tunajenga jamii zenye ustaarabu zaidi, na katika kufanya hivyo tunakumbana na magonjwa ya maendeleo. Kwa upande mmoja tumepata mafanikio makubwa sana katika sayansi na teknolojia na tumeongeza wastani wa umri wa kuishi wa binadamu na kiwango chake cha afya. Kwa upande mwingine idadi ya watu duniani imeongezeka kutoka bilioni 1.9 mwanzoni mwa karne iliyopita na kufikia zaidi ya biloni 6 hivi sasa. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa idadi hiyo itafikia bilioni 8 kunako 2025.
Matatizo ya kimazingira, vita, kuzidi idadi ya watu, ukosefu wa elimu na kasi kubwa ya maendeleo yote yanatukabili, lakini tatizo kubwa la jumla ni afya. Tukizungumzia kuhusu watu wenye afya nzuri, tunazungumzia robo tu ya watu dunuiani. Watu wenye matatizo ya kukithiri ya kiafya wanachukua robo ya watu duniani. Nusu iliyobakia ina tatizo la afya duni. Na asilimia 60 hadi 70 ya watu hawa wenye afya duni wanaugua maradhi yanayotokana na maendeleo, kama presha ya kupanda, kuziba mishipa ya damu, matatizo ya moyo, saratani, endocrine disease, na baadhi ya magonjwa yanayopunguza kinga za binadamu kama UKIMWI.
Takwimu za karibuni kutoka majumbani na vyanzo vya kimataifa zinaonyesha kuwa kuna vifo na ulemavu mwingi kwa sababu ya kuongezeka kwa magonjwa haya.
Presha Ya Kupanda (Hypertension)
Kuonekana kwa tatizo hili kunazidi asilimia 20 kwenye nchi za magharibi. Katika nchi ya China, takwimu kutoka kwa watu 950,000 zilionyesha kuwa asilimia 11 ya watu wenye umri unaozidi miaka 15 walikuwa na tatizo hili, watu wa umri wa kati na wenye umri mkubwa wakiwa zaidi ya nusu ya namba hiyo.
Magonjwa Ya Moyo
Ugonjwa huu ndio unaoongeza kwa kuua watu duniani. Vifo vya watu vinavyotokana na ugonjwa huu vinazidi milioni 12 kwa mwaka. Katika nchi ya China, kuna watu wapatao milioni 15 wenye maumivu ya vifua yanayotokana na dosari katika moyo (angina) na vifo vipatavyo milioni 1 hutokea kila mwaka.
Magonjwa Ya Mishipa Ya Ubongo (Cerebral-vascular disease)
Huu ni ugonjwa wa pili kwa kusababisha vifo katika nchi ya China. Vifo vinavyotokana na ugonjwa huu kwa mwaka ni milioni 1.5 na watu wapatao tatizo hili ni milioni 1.52 kwa mwaka. Katika nchi ya China watu wanaougua ugonjwa huu watafikia milioni 53 katika miaka kumi ijayo.
Kansa
Kansa au saratani imekuwa ndio ugonjwa unaongoza kwa kusababisha vifo kuanzia mwaka 1990. Watu wanaokufa kwa ugonjwa huu kwa mwaka ni milioni 1.52. Wagonjwa wa saratani katika nchi ya China watakuwa zaidi ya milioni 30 katika miaka 20 ijayo.
Kisukari
Katika nchi ya China, wagonjwa wa kisukari tayari wamefikia milioni 15 na inakadiriwa kuwa idadi hiyo itafikia mara mbili katika miaka 15 ijayo.
Shirika la Afya la Dunia (WHO) linaelekeza kuwa kila mmoja wetu anahusika katika kuboresha afya zetu. Kulifikia lengo hilo, hatua ya kwanza ni kuwaelimisha watu kuwa afya na kinga ni vitu ambavyo havikwepeki katika shughuli zao za kawaida. Hatua ya pili ni kutafakari kwa makini ugunduzi wa kisayansi. Katika karne hii tuliyoko, watu wanadhamiria kutunza afya zao na kuzuia maradhi.
Kampuni ya Green World imetengeneza mlolongo wa bidhaa kwa lengo la kupunguza mafuta ndani ya mwili, kupunguza kudhoofika kwa mwili na akili kunakoambatana na umri, kupiga vita kansa, na kuweka sawa kinga za mwili. Tangu walipoanza kazi hii, mamilioni ya watu wamenufaika na bidhaa hizi.