Propolis Capsule
Viungo:
Propolis, Radix Ginseng, Vegetable Oil
Kazi Na Faida Zake
- Kuangamiza na kuzuia kukua kwa bakteria wa aina nyingi na maambukizi ya virusi
- Kuinua kiwango cha lishe na afya kwa ujumla
Inafaa Kutumiwa Kwa:
- Watu wenye maambukizi sugu (bakteria, fungus na virusi)
- Watu wenye upungufu wa kinga za mwili
- Watu wenye matatizo ya kukauka kwa koo, matatizo ya conjunctiva za macho (conjunctivitis), sinus congestion, mafua, influenza, bronchitis, matatizo ya masikio, matatizo ya fizi na eneo linalozunguka meno, pneumonia, maambukizi kwenye nyongo, vidonda vya tumbo, maambukizi ya njia ya mkojo, matatizo ya utumbo na magonjwa ya ngozi.
Maelezo Muhimu:
Thamani Ya Propolis Katika Virutubisho:
Kuna aina zaidi ya 30 ya michanganyiko ya flavones, aina mbalimbli za terpenes, tindikali za amino 20, vitamini mbalimbali, vimeng'enya hai, elementi adimu kama chuma, chrome, zinc, selenium, magnesium, calcium, phosphorus, n.k. Propolis pia ina aromatic acids 10, aromatic esters 30, zaidi ya aina 30 ya mafuta. Polysaccharides zilizomo ndani ya propolis ni muhimu kwa mwili.
Historia Ya Propolis:
Propolis ina historia ya kutumika kama dawa kwa miaka mingi, kuanzia miaka ya 350 BC, wakati wa uhai wa Aristotle. Wagiriki waliitumia propolis kwa ajili ya majipu; watu wa Assyria waliitumia kwa ajili ya kuponya vidonda na uvimbe; watu wa Misri waliitumia propolis kwa ajili ya kutunza maiti isioze (mummification). Bidhaa hii ya asili ya nyuki inasifika kama dawa ya kuponya magonjwa yote "elixir" na "antibiotic asilia". Miaka 1900 iliyopita kitabu kilichoandikwa na warumi "History of the Nature", kilitaja kwa undani vyanzo na faida za propolis.
Tabia ya Kuzuia Vyanzo Vya Magonjwa (Antiseptic and Antimicrobial Properties)
Utafiti unaonyesha kuwa ina tabia ya kuua wadudu wa magonjwa, ni antibiotic, inazuia na kuua fungus, na hata kuua baadhi ya virusi. Propoilis ni kinga ya kwanza ya asili. Ina nguvu sana ya kufanya kazi, na mara nyingi huitwa Russian penicillin kwa kutoa kumbukumbu ya kazi kubwa ya tafiti zilizofanyika nchini Urusi kutoka kwa nyuki. Propolis inaonyesha kufanya kazi nzuri ya kuzuia na kuua bakteria wa aina mbalimbali na maambukizi ya virusi. Hata bakteria wa aina ya streptococcus wanaonyesha kudhibitiwa na propolis.
Kuongeza Kinga:
Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa watu wanaotumia propolis mara kwa mara hawadhuriki na mafua ya kipindi cha baridi na wanaonyesha kujenga kinga dhidi ya virusi wa kawaida, ikiwa ni pamoja na aina kadhaa za virusi wanaosababisha mafua.
Antibiotic Asilia:
Antibiotic za kemikali zinaua bakteria wote mwilini, bakteria rafiki wanaohitajika ili mifumo ya mmeng'enyo ya chakula ifanye kazi zao vizuri na bakteria wabaya wanaoishi kwenye matumbo.
Mtu anayeandikiwa antibiotic ya aina fulani na kuitumia mara nyingi kwa kuua bakteria kwa matatizo ya aina tofauti baadaye atakuja kujifunnza kuwa antibotic hiyo haifanyi tena kazi vizuri kama ilivyokuwa ikifanya kazi mwanzoni. Wadudu wadogo wavamizi taratibu wanakuwa wamejenga uwezo wa kushindana na antibiotic inayotolewa. Propolis, ambayo ni antibiotic asilia, inafanya kazi dhdi ya bakteria waharibifu bila ya kuwaangamiza bakteria rafiki ambao wanahitajika na mwili.
Kufanya Kazi Nyingi:
Propolis imeonyesha kufanya kazi vizuri dhidi ya vizazi vya bakteria ambavyo vimekuwa sugu kwa tiba ya kutumia antibiotics za kemikali. Maeneo ya kutumia tiba ya propolis ni mapana sana. Yanajumuisha kansa, maambukizi ya njia ya mkojo, kuvimba kwa koo, gout, vidonda vya juu ya mwili, sinus congestion, mafua, infulenza, bronchitis, gastritis, magonjwa ya masikio, magonjwa na fizi na meno, maambukizi ya utumbo, vidonda vya tumbo, milipuko ya vimeng'enya, pneumonia, arthritis, magonjwa ya mapafu, virusi wa tumboni, maumivu ya kichwa, ugonjwa wa Parkinson's, maambukizi kwenye nyongo, sclerosis, matatizo ya mzunguko wa damu, warts, conjuctivitis, na sauti kukwaruza.
Tahadhali:
Haifai kwa watoto wadogo, vichanga, wanawake waja wazito au watu wenye mzio wa asali na bidhaa za asali. Tumia nusu ya dozi kwa kundi la watoto wa miaka 10 hadi 18.
<<<<< MWANZO