Nutriplant Organic Plus Fertilizer
Sifa Zake
Bidhaa hii yenye uwingi wa molekuli za amino acids, peptides na chelates ni namna ya lishe ya asili kwa mimea. Haina sumu ni salama kwa mazingira, huipa mimea (mboga, miti ya matunda, maua, na nafaka) virutubishi mbalimbali.
Kazi na Faida zake
- Husaidia ukuaji wa mizizi, mashina na majani ya mimea;
- Huongeza ubora na ladha ya sehemu za mimea zinazovunwa;
- Huongeza uwezo wa mimea wa kuvumilia ukame, uwezo wa uzalishaji, kupambana na wadudu na magonjwa;
- Husaidia mbegu kuota haraka na kuwa na nguvu;
- Huboresha mwundo na utendaji wa ardhi.
Maelezo Muhimu
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameonyesha kuwa mmea unaweza pia kupata chakula chake kupitia majani na ukawa kamilifu kabisa. Matokeo ya ugunduzi huo umetuletea aina mpya za mbolea. Mojawapo ya mbolea hizo mpya ni mbolea ya maji inayoitwa Mbolea - green worldNutriplant Organic Plus Fertilizer (NOPF) inayotengenezwa na kampuni ya Green World.
Mbolea hii inatunzwa ndani ya plastiki ndogo yenye ujazo wa lita moja na hutumika kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea. Utengenezaji wa mbolea hii umezingatia mahitaji yote ya mmea ikiwa ni pamoja na virutubishi vyote vinavyohitajika kwa wingi na mmea (macronutrients) ambavyo ni Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Calcium, magnesium na Sulphur, na vyote ambavyo vinayohitajika kwa kiwango kidogo (micronutrients), vikiwa ni Ferrous, Zinc, Copper, Boron, Manganese, Silicon, Molybdenum, Sodium, Cobalt na Chlorine.
Kwa vile amino acids ni muhimu katika ukuaji wa mmea, mbolea hii imejumuisha aina zote 18 za amino acids. Pamoja na ukuaji wa mmea, amino acids huupa mmea sifa nyingine nyingi sana, mfano; uwezo wa kupambana na magonjwa na wadudu, ukuaji wa haraka n.k.
Mbolea za nitrates, sulphates na phospahtes hutengenezwa viwandani, kwa hiyo ni mbolea za kemikali. Mbolea hizi kiutaalamu huitwa Inorganic Fertilizers. Aina hii mpya ya mbolea inayotengenezwa na Green World, haitokani na kemikali bali na wanyama na mimea. Organic maana yake kitu kilichotokana na viumbe hai – kitu kinachotokana na mimea au wanyama. Kuna tofauti kubwa kati ya kutumia mbolea za kemikali na mbolea za organiki. Tofauti kuu ni:
1. Mbolea ya Green World ina virutubishi vyote, vile vinavyohitajika kwa wingi na mmea (macronutrients), na vile vinavyohitajika kwa kiwango kidogo (micronutrients). Mbolea za kemikali hutengenezwa zikiwa na macronutrients tu, pengine moja au mbili.
2. Mbolea za Green World ni rafiki wa mazingira. Wakati ukiendelea kuitumia mbolea hii, mazingira yako hayaharibiki tofauti na matumizi ya mbolea za kemikali ambazo huharibu mazingira.
3. Mbolea za Green World zinatumika kwa muda mrefu na kuendela kukuletea mazao bora wakati mbolea zingine hutumika kwa muda mfupi kabla ya kuanza kudorora kwa uzalishaji.
4. Mbolea za Green World huongeza ubora wa mazao, kama ukubwa, rangi, ujazo na ladha. Mbolea nyingine za kemikali hupunguza ubora wa mazao.
5. Mbolea za Green World huboresha udongo wa shamba lako. Unaweza kuitumia kutibu ardhi iliyochoka. Mbolea hii hurudishia pH ya udongo hadi kiwango kinachohitajika na mimea cha kati ya 6-8. Mbolea za kemikali huzidisha pH ya udongo, hatimaye kuufanya udongo wa shamba lako kuwa haufai kwa mimea.
<<<<< MWANZO