Multi-Vitamins Tablet (for adults)
Viungo:
Vitamin A (1167 IU), Vitamin B1 (900ug), Vitamin B2 (900 ug), Vitamin B6 (900ug), Vitamin B12 (0.9ug), Vitamoni C (40mg), Vitamin D
(180 IU), Vitamin E (500ug), Folic Acid (100 ug), Niacin (7 mg)
Kazi Na Faida Zake
Multivitamin huweka vizuri shughuli za kimetaboliki na utendaji kazi wa mwili. Vidonge vya Multivitamini vya Green World vina vitamini zote muhimu kwa mwili. Matumizi ya bidhaa hii ya kila siku yanaweza kukidhi mahitaji ya mwili ya vitamini kwa watoto na watu wazima.
Yafaa Kwa:
- Watu wenye upungufu wa vitamini
.
Multi-Vitamins Tablet (for children)
Akina mama wanajua jinsi ilivyo vigumu kumfanya mtoto ale chakula kinachojitosheleza ambacho ndicho chanzo kikuu cha vitamini na madini. Watoto wanavihitaji virutubishi hivi muhimu ili wawe na kinga za mwilli imara na waweze kukua vizuri kimwili na kiakili. Kwa bahati mbaya si watoto wengi wanaopata vitamini zote kupitia chakula chao. Ukosefu wa vitamini hizo unawafanya wachelewe kukua na mara nyingine kupata magonjwa mabaya.
Maelezo Muhimu:
. Ukosefu wa vitamini kwa watoto
Vitamini A - ni vitamini ya jicho. Kama mtoto anatazama TV kwa muda mrefu, au kama anakaa mbele ya kompyuta mara kwa mara, macho yake yanatumia sana vitamiii A. Ukosefu wa vitamini A unasababisha kutokuona vizuri, ukuaji dhaifu na upungufu wa kinga za mwili.
. Vitamini B.
Watoto wanaokula sana peremende wanaweza kupungukiwa vitamini B, kwa sababu vitamini hizi huharibiwa kirahisi sana na sukari. Vitamini B ni muhimu sana katika utendaji kazi wa mfumo wa neva na ni muhimu vile vile katika shughuli za kimetaboliki za wanga. B6, B12 , folate na hasa vitamini B1 ni muhimu sana kwa ubongo wa mwanao na ukosefu unaweza kusababisha kushindwa kutuliza akili na upungufu wa kumbukumbu.
. Vitamini C. Matunda na mboga za majani ndivyo vyenye uwingi wa vitamini C na watoto wengi wana upungufu wa vitamini C kwa sababu hawali sana vitu hivi. Kupenda sana vitu vya viwandani kunawafanya watoto wengi kukosa vitamini C. Watoto wanaopata mafua au maambukizi mara nyingi wanaweza kuwa na upungufu wa vitamini C, kwa sababu ni ya muhimu katika kuimarisha kinga zao za mwili. Vile vile, vitamini hii ni ya muhinu katika ukuaji wa kawaida, uponyaji wa vidonda na afya ya fizi.
. Vitamini E. Theluthi mbili za watoto hawapati vitamini E kwa kiwango cha kutosha.Vitamini E ni antioxidant yenye nguvu na muhimu katika kuzuia saratani na magonjwa ya moyo. Ukosefu wa vitamini hii kwa watoto husababisha ukuaji mbovu na pengine ukosefu wa damu ya kutosha.
<<<<< MWANZO