Lecithin Capsule
Viungo:
Lecithin asilia kutoka Soya
Kazi na Faida zake:
- Kiungo muhimu cha ngozi izungukayo seli;
- Kuimarisha mfumo wa neva na kuboresha ubongo;
- Kupunguza kiwango cha lipids katika damu kwa kubadilisha LDL kuwa HDL;
- Kulilinda ini na kusaidia ufanyaji kazi wa ini.
Yafaa kwa:
- Watu wanaohitaji kuboresha kumbukumbu na umakini wa ubongo
- Watu wenye uwingi wa lipids katika damu, matatizo ya moyo na ubongo
- Watu walio katika hali mbaya au wenye matatizo ya muda mrefu ya mafuta kwenye ini, homa ya ini (hepatitis) na liver cirrhosis.
Maelezo Muhimu:
Jina la LECITHIN linatokana na neno la kigiriki "lithos" .... lenye maana ya kiini cha yai. Uwepo wa lecithin ndani ya kiini cha yai kunaonyesha umuhimu wake katika UKUAJI. Wanasayansi na wataalamu wa mambo ya lishe wamethibitisha kuwa soybean lecithin inasaidia afya na kusaidia kuzuia maradhi. Lecithin hupatikana kutoka kwenye mayai, samaki (salmon), nyama (organ meat) na soya.
1. Lecithin ni mlinzi wa seli: Lecithin ina phospholipid. Kama phospholipids hazitakuwepo kwa kiwango cha kutosha ili kutunza umbo la nje la seli (cell membrane structure), ngozi ya nje ya seli itapungukiwa uwezo wake wa kuilinda seli na kusafirisha virutubisho nje na ndani ya seli. Kadiri mwili utakavyokuwa na uwingi wa lecithin, ndivyo utakavyokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuvunjavunja chakula, kuwa na kinga zaidi, kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kujizalishia seli mpya kuchukua nafasi ya seli zinazokufa. Lecithi ni kiungo muhimu cha kila seli katika mwili. Ni muhimu katika ujenzi wa seli na kuzuia seli zisiwe kavu. Seli zikiwa na afya, mwili utakuwa na afya.
2. Huulinda moyo na mishipa ya damu: Lecithin huyeyusha mafuta na kuyaacha yaelee ndani ya damu, huyazuia mafuta hayo kunata kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu. Vipande vya mafuta vikishindwa kunata kwenye eneo lo lote la mwili, husafirishwa hadi kwenye ini ambako huvujwavunjwa na kutoa nguvu mwilini. Kuboreshwa kwa mzunguko wa damu hutokana na nyongeza ya lecithin inayozuia kuganda kwa damu (blood clots) na kuboresha afya aya ini. Kwa kufanya hivyo, lecithin inazuia magonjwa ya shinikizo la damu (high blood prssure), kupungua kipenyo cha mishipa ya damu (Atherosclerosis), kiharusi na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases).
3. Huboresha afya ya ubongo:Lecithin hutengeneza ACETYLCHOLINE, kiungo muhimu katika kusafirisha ujumbe kutoka neva moja hadi nyingine. Kwa hiyo lecithin inazuia na kusaidia uponyaji wa magonjwa ya kupoteza kumbukumbu, kudorora kwa afya ya ubongo (dementia), ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na kufuatiwa na kushindwa kufikiri, kushindwa kuongea na mwisho kushindwa kufanya lo lote (alzheimer's).Lecithin ni chakula bora kwa kujenga akili na kurudisha kumbukumbu (Brain care food).
4.Hulinda Ini: Lecithin hutumika na ini katika kutengeneza nyongo. Lecithin huzuia na kusaidia kuondoa matatizo ya kuwa na mawe kwenye nyongo (gallstone), ini kuwa na mafuta (fatty liver) na ugonjwa wa ini kuwa na nyuzinyuzi (hepatic cirrhosis.)
5.Hulinda utumbo: Ngozi inayotanda juu ya utumbo mdogo ni moja ya viungo vinavyokua kwa haraka sana katika mwili, hujijenga upya kila baada ya siku moja na nusu. Lecithin husaidia katika ujenzi wa kuta za utumbo. Kwa hiyo lecithin husaidia kuondoa maumivu ya kwenye utumbo mpana (colitis). ugonjwa ushambuliao utumbo mdogo na kusababisha kuharisha na maumivu (Crohn's disease).
Ni rafiki wa Akina mama: Lecithin ni muhimu katika uzalishaji wa homoni mbalimbali zinazosimamia utoaji jasho. Lecithin ni bidhaa ya kusaidia ngozi isikauke. Lecithin inazuia na kusaidia tatizo la kupata maumivu kabla ya hedhi (Pre-menstrual syndrome -PMS-), matatizo yanayoambatana na kukoma hedhi na kusaidia kupata usingizi.
<<<<< MWANZO