Mwongozo Wa Biashara Ya Mtandao Ya Kampuni Ya Green World Kwa Afrika Mashariki

kusajili wanachama


Mbinu Za Kuuza Na Kusajili Wanachama

Ili kuweza kujenga kikundi cha wauzaji wa bidhaa za Green World, unapaswa ujue namna ya kusajili wanachama wapya. Kumbuka kuwa huwezi kupata pesa yo yote kutoka Green World kama hakuna mauzo ya bidhaa au huduma za Green World. Green World inakuwezesha kupata mafanikio kwa kukupa misaada ya namna nyingi sana - video za kuitangaza kampuni, vitu vya kukupa motisha, machapisho, n.k. na watu watakaokusaidia kuweza kuzielewa bidhaa za kampuni, mpango wa malipo na fursa nyingine zilizopo. Mwanachama makini hataishia kusajili wanachama wapya tu bali atamsaidia na kumfundisha kila aliyemsajili ili aweze kuwa mwanachama mwenye mafanikio na hatimaye nao waweze kuwafundisha wale watakaowasajili. Matokeo ya kusajili na kutoa mafunzo kamili kwa kila anayesajiliwa ni "URUDUFU" (duplication): kuwafanya wafuasi wako waelewe na kufuata njia yako ya mafanikio. Tabia hii ikiendelezwa kizazi hadi kizazi huleta - mlipuko wa mafanikio yako kutokana na mafanikio ya wale uliowafundisha na ambao baadaye waliwafundisha wengine kupata mafanikio.

Mwanzo Wa Mchakato: Kuuza Bidhaa

Ili kuwa mwanachama halisi wa Greeen World

1. Kujaza na kurejesha fomu ya maombi ya uanachama ikiambatanishwa na ada ya uanachama 2. Maombi kukubaliwa na Green World

Wakati ukiendelea kufanya kazi na wanachama uliowasajili, angalia kwa makini video ya Green World na pitia kwa makini zana nyingine za mafunzo. Wahamasishe kuielewa na kuitumia nadharia ya mwendelezo au urudufu (duplication) - kwa kufuata njia zako za mafanikio na kuelewa nadharia ya mfumko wa mafanikio (multiplication) - unaotokana na kujijengea tabia toka awali ya kutoa mafunzo kwa wanachama wapya na kujitengenezea mtindo wako wa mafunzo utakaounda jumuia ya wafanyabiashara ya aina yako ya kipekee.

Mafanikio yako yanaanza na wewe. Kwa kuwaeleimisha na kutoa fursa ya Green world kwa watu walio karibu na wewe, unaanza kujijengea biashara yako

Pamoja na kupata faida ya rejereja, unahitaji kuhakikisha kuwa unajenga kikosi madhubuti kitakachouza bidhaa na huduma za Green World.

Biashara ya rejareja ni pamoja na: