Mwongozo Wa Biashara Ya Mtandao Ya Kampuni Ya Green World Kwa Afrika Mashariki

Kuratibu Biashara Yako Ya Green World

biashara ya nyumbani.png


Hapa chini tunaorodhesha hatua 10 ambazo tunashauri uzifanyie kazi ili kuwa na biashara yenye mpangalio utakaokuletea mafanikio na faida.

Fungua Akaunti Ya Benki Ya Kipekee

Haifai kuchanganya pesa zako binafsi na pesa za biashara. Uwezekano wa kufanya kosa na kuchanganya mahesabu utakuwa ni mkubwa sana. Vile vile inafaa kutofautisha matumizi ya biashara na matumizi yako binafsi.

Agiza Business Cards Na Stationery

kitambulishoTumia kadi za biashara (business cards) na karatasi zenye nembo ya Green World zilizothibitishwa na
kampuni ya Green World.


Hakikisha kuwa watu wanakufahamu na wanajua ni nini unaweza kuwafanyia kwa kuwaachia kadi zako za
biashara.

Utambulisho Wa Green World

Jitambulishe kwenye jamii yako kuwa wewe ni mfanya biashara wa kampuni ya Green World:

Andaa Ofisi Yako

ofisi binafsi ya nyumbani Uzuri mmoja wa kampuni ya Green World ni kwamba inakuruhusu kufanya biashara kutoka nyumbani kwako. Hii ina maana kuwa huna haja ya kwenda kutafuta chumba cha biashara cha kupanga. Unahitaji kutumia gharama ndogo sana kuiendesha biashara hii. Unachohitajika kufanya
ni kutenga sehemu ndani ya nyumba yako kwa ajili ya biashara au kuweka duka. Jitenge na masuala ya kifamilia ukiwa kazini.

Usipoweza kujitenga na masula ya kifamilia wakati ukiendelea na biashara yako ya Green World, utakosa mafanikio ya kuridhisha kutokana na kukatishwa katishwa na wanafamilia. Vile vile hutaweza kujua kwa uhakika ni kiasi gani cha muda wako unakiwekeza kwenye biashara na mafanikio yako ndani ya Green World.

Tengeneza Kalenda Yako

Pamoja na kujitengea sehemu ya kufanyia kazi zako, ni lazima uwe na ratiba ya kukuongoza ni muda gani utakuwa ukifanya kazi za biashara yako ya Green World. Jipangie ni saa ngapi utazitumia katika kujenga biashara yako ya Green World. Kumbuka njozi zako za mafanikio, na hakikisha unajiwekea muda wa kutosha kila siku ili kuyafikia malengo yako.

Panga ratibu na ifuate kikamilifu!

Kupata mafanikio ya ukweli, ratiba yako lazima ionyeshe ni muda wa saa ngapi umeutenga kwa ajili ya kufanya shughuli za biashara yako ya Green World kila siku. Kumbuka kuwa wewe ndiye mkurugenzi wa biashara yako - hakuna mtu wa kukufuatilia umeanza kazi saa ngapi, hakuna wa kukuhimiza wala kukuadhibu kama hutofanya kazi. Ni kitu kizuri sana! Lakini lazima uwe na mpango na kuufuata mpango huo, kwamba utafanyia wapi kazi zako na kwa muda gani. Kwa mfano saa 1 hadi saa 4 usiku siku za Jumanne, Jumatano, na Alhamisi, na saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri siku za Jumamosi. Weka alama ya siku hizo kwenye kalenda na itundike kalenda hiyo mahali ambapo utaiona kiurahisi kila siku. Kisha, jenga tabia ya kufuata utaratibu wako. Kufikia malengo, ni lazima ujue ni kwa nini unafanya kazi.

Ukishajiwekea mpango wako wa kufanya kazi na kuanza kuufuata, ni vizuri kuufanyia tahmini kila wakati na kufanya marekebisho. Mipango ya kazi inafanya kazi vizuri pale inapofuatwa, kufanyiwa tahmini na kurekebishwa mara kwa mara.

Tunza Kumbukumbu Sahihi

Utunzaji wa kumbukumbu ni kitu muhimu katika mafanikio ya biashara yako. Kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi yako ni kitu muhimu katika kupima mafanikio yako. Kila mwezi utapata karatasi (printout) itakayokuonyesha wanachama wa vizazi vya chini yako. Karatasi hii itaonyesha ni nani walio katika jumuia yako ya wafanyabiashara wa kampuni ya Green World na katika mikondo (miguu) gani ya chini yako. Ripoti hiyo pia itakuonyesha ukuaji na shughuli za jumuia yako ya wafanyabiashara, ikikuonyesha sehemu ambazo unahitaji kuziwekea mkazo katika kukuza biashara yako.

Mahitaji

Mengi ya mahitaji yako tayari unayo. Weka orodha ya mahitaji unayotakiwa kuwa nayo kila wakati - kuanzia karatasi hadi vipeperushi. Vinunue na uwe navyo tayari. Kuwa na vifaa vya ofisi vya kutosha, kuwa na nyenzo za kufundishia na kufanyia matangazo (video,vipeperushi, n.k.) za kutosha, kunaleta tofauti kubwa katika uharaka wa mafanikio ya biashara yako.

Line Ya Simu Ya Kipekee

Unaweza baadaye kuhitaji kuwa na line ya kipekee ya simu kwa ajili ya kufanyia mawasiliano yako ya kibiashara

Endesha Biashara Ya Green World Kama Biashara

Kuna faida nyingi za kuendesha biashara ya Green World kutoka nyumbani kwako - kufanya kazi kwa muda uliojipangia, kuishi maisha unayopenda, kujipangia mipango yako ya baadaye .... na pengine unafuu wa kodi. Lakini faidi hizi zote zinaweza kugeuka hasara kama utaweka mzaha kwenye biashara yako. Kutokuwepo mtu wa kukuuliza umefika saa ngapi kazini haimaanishi usifanye kazi kwa muda unaotakiwa. Uhuru wa njia ya mafanikio ni uhuru wa kushindwa pia. Ni nini kitaleta tofauti? Ni kuonyesha ukomavu kitaaluma.

Maono Ya Baadaye

Fikiria unataka biashara yako iwe imefikia wapi katika miezi sita inayokuja, baada ya mwaka mmoja, miaka mitano, miaka kumi. Andaa malengo yako ya muda mrefu kisha yagawe kwenye malengo ya muda mfupi. Jenga picha ya mafanikio yako!

maono ya kibiashara.png

Kuiendesha vizuri biashara yako kunaweza kuwa moja ya vitu vya kukupa tija kubwa ndani ya Green World. Kufanikisha mafanikio ya biashara hii kutakupa faraja kubwa! Kumbuka kuwa utafanikisha biashara yako na Green World endapo:

  • Utahudhuria mafunzo na kufuata taratibu za kampuni
  • Utaielewa kampuni ya Green World
  • Utafuata ratiba zako ulizojiwekea kwa umakini
  • Ofisi yako ya nyumbani ya Green World ina lengo la kukuletea mafanikio. Kampuni itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa biashara yako inapata mafanikio.





    <<<< MWANZO