Mwongozo Wa Biashara Ya Mtandao Ya Kampuni Ya Green World Kwa Afrika Mashariki

Hatua Za Kufikia Mafanikio

mafanikio ndani ya green world

Kuweka Malengo

Watu wote waliopata mafanikio makubwa wamekuwa wakijiwekea malengo na kukazana kufanya kazi kuyafikia malengo yao - wanajua wanapotaka kupafikia. Wewe pia unaweza kujiwekea malengo na kuonja msisimko utakaoupata pale utakapoyafikia malengo yako .... hata kama ulishawahi kukatishwa tamaa kabla kwa kujiwekea malengo. Katika biashara yako ya Green World, kujiwekea malengo na kuyapitia kila wakati ndiko kunakoleta tofauti kati ya mafanikio MADOGO na mafanikio MAKUBWA ambayo mtu anaweza kuyapata. Malengo mengi hayafikiwi kwa sababu huwa hayafafanuliwi au huwa hayaelekezwi kwenye kitu maalumu. Ukizingatia misingi na fikra za Green World - ukianza kuyafikiria malengo yako kama shughuli za kawaida na kama hatua za kukutoa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine unayotoka kuifikia - utaanza kujenga ari na kuuzoea mfumo utakaokusaidia kuyafikia malengo yako.

Hatua ya kwanza katika kufanikisha jambo lo lote ni kuamua ni nini unachotaka kukifanya.


Amua Unachotaka Kukifanya


Kwanza amua ni nini unahitaji kifanyike - siyo mwakani au miaka 10 ijayo, bali mwezi huu na mwezi ujao.

Mpango wa mafunzo ya biashara wa Green World unalenga kufikia lengo maalumu. Kwanza unafundishwa kuorodhesha watu ambao unataka kuwashirikisha katika kutumia bidhaa na kuwasajili kuwa wanachama. Kisha unaelekezwa kutoka na kwenda kuwaelezea walengwa hao kuhusu fursa ya Green World. Malengo rahisi yanayotekelezeka na kujenga uwezo mkubwa wa kufikia mafanikio. Na kwa vile Green World imejengwa kwenye mpango wa malipo ulio bora, nguvu zako ndogo na uwajibikaji wako vitakuletea matokeo makubwa kuzidi kabisa ulichokiwekeza.

Kwa hiyo anza kwa kutengeneza orodha - orodha ya kwenye maandishi. Malengo ambayo hayakuandikwa ni kama njozi. Fafanua ni kitu gani uanchokihitaji. Kadri unavyokuwa mwazi na kuandika malengo yako kwa usahihi zaidi, ndivyo yamkini kuwa utayafikia itakavyoongezeka. Tuseme kwa mfano maahitaji yako ni kipato cha ziada, andika ni kiasi gani umepanga kukipata..... andika vizuri ni saa ngapi kwa wiki utawekeza kwenye biashara hii ili kuyafikia malengo yako na panga vizuri ratiba yako ya biashara- utafanya nini weekends, jioni au asubuhi?


Kuwa Na maono


kuweka malengo

Kuwa na maono hapa tunamaanisha zaidi ya kuwa na picha katika jicho la ubongo wako ya kile kitu unachokitaka. Unatakiwa kuanza kuona kuwa umefanikiwa kukifia na kukihodhi kile kitu ambacho umekuwa ukikifikiria. Inatakiwa uanze kuamini na kujiona kuwa ni yule mtu uliyekuwa umenuia kuwa. Siyo njozi sisizo na maana kwani wanasaikolojia wanatueleza kuwa watu wanaoanza kuamini na kuwa na tabia ya mtu mwenye mafanikio, wana nafasi kubwa sana ya kufanikwa kiukweli.


Weka Mkakati Wa Kufikia malengo


Nyumba kabla ya kuanza kujengwa, ramani huandaliwa ikionyesha vipengele vyote vya ujenzi. Hivyo hivyo, katika biashara yako lazima ujue ni nini unahitajika kufanya ili kufikia malengo yako. Jiwekee malengo ya muda mfupi na panga tarehe za kukamilisha malengo hayo. Kwa mfano, kama umepanga kufikia lengo fulani katika miezi miwili, gawanya kipindi hicho katika wiki 8 kisha panga malengo madogo ya kufikiwa katika kila wiki katika hizo 8. Mwisho ili kufikia malengo ya kila wiki, panga ni nini utafanya kila siku ili kuyafikia malengo ya wiki. Ni kiasi gani cha bidhaa utatakiwa kuuza kila siku? Ni wanachama wangapi utawasajili na kuwafundisha ili mafanikio yao yachangie kufanikwa kwako?

Kufikia mafanikio inachukua muda. Jipe moyo na amini kuwa utapata furaha katika hatua unazozichukua. Usiache kujipongeza pale unapofanikisha jambo ambalo linakusogeza zaidi kwenye njia yako ya kukamilisha ndoto zako. Mwone kiongozi wa juu yako na mweleze kuhusu mafanikio yako, kwa vyo vyote naye atakupongeza.


Zoezi La Kupanga Malengo


Katika kupanga malengo ni muhimu kutumia kanuni ya SMART ambacho ni kifupi cha maneno ya kiingereza: Specific, Measurable, Achievable, Realistic na Timely. Itumie kanuni ya SMART kupata malengo yalioandaliwa vizuri na yenye kutoa ari. Katika kukumilisha zoezi hili utahitaji peni au penseli na karatasi. Ili kupata mafanikio malengo yako lazima:


Hatua 1


Juu ya karatasi nyeupe andika vitu unavyohitaji kuvifanya. Chagua kimoja kwenye orodha hivy kisha kizungushie duara. Kichambue na kukielezea kwa undani.


Hatua 2


Jione kuwa unapata na kufurahia kitu unachokihitaji. Usiogope kuiremba ndoto yako na vitu vingine unavyovifikiria. Jipangie muda katika wiki hii hii kutoka na kwenda kukiona kitu cha ndoto yako. Tafuta taarifa zikiwemo za kimaandishi kuhusu kitu hicho. Weka picha ya kitu hicho mahali ambapo kila wakati kitakukumbusha. Unaweza kupata kitu unachokiwazia na kuamini kuwa utapata.


Hatua 3


Andika vitu unavyohitajika kuvifanya ili kufikia lengo lako - Ni idadi gani au ni nyenzo zipi za Green World unahitaji kuwashirikisha wengine? Na nani? Ni idadi gani ya wanachama wa Green world unahitaji kusajili na kuwafundisha na vitu gani watahitaji ili mafanikio yao yachangie kwenye mafanikio yako? Panga ratiba ( siku, wiki, miezi, miaka) ya kufanikisha lengo lako. Sasa ..... yafanye malengo yako kuwa ya kweli kwa kuyaandika chini. Wajibika kutimiza malengo yako!


Hatua 4


Furahia kuyakamilisha malengo yako!

Kuwasiliana

Watu wanaamini zaidi pale wanapopata maelezo kutoka kwa mtu ambaye ana uzoefu wa kitu anachokielezea. Tumia uzoefu wako kuelezea ubora wa bidhaa za Green World na kuhusu fursa hii ya biashara. Kuna usambazaji wa taarifa usio rasmi, huu unatokea pale unapokuwa na mazungumzo ya kawaida tu na watu wa ndani ya familia au marafiki. Usiache kupanda mbegu ambazo baadaye zinaweza kukuletea mavuno makubwa. Utoaji taarifa rasmi ni ule unaofanyika pale unapofanya presentation ya mtu mmoja au ya kundi. Hapa taarifa inayotolewa huwa imeandaliwa vizuri zaidi kuliko ile inayotolewa kwenye mazungumzo ya kawaida.

Unapotoa maelezo yo yote kuhusu ubora wa bidhaa au fursa ya Green World, hakikisha kuwa unafuata maadili, sheria na taratibu kuhusu madai:

. Sitatoa madai yo yote kuhusu bidhaa au huduma za kampuni ya Green World zaidi ya yale ambayo yamewekwa kimaandishi na kampuni. Sitasahau kuwa maelezo yangu binafsi kuhusu uzoefu wangu wa bidhaa na huduma za kampuni ya Green World ni nyongeza yangu ya faida za bidhaa na huduma za kampuni ninazozitumia kuitangaza biashara.

. Sitatoa madai yo yote kuhusu malipo au vielelezo vya mpango wa malipo wa kampuni ya Green World, nikielewa kuwa matokeo ya mapango wa malipo wa Green World ni nadra kutokea. Hakuna timu inayokua na kujijenga kikamilifu na kwa hiyo si rahisi kubashiri matokeo ya mapato. Isitoshe, mafanikio ya mwanachama wa Green World yanategemea vitu vingi vikiwemo, muda na nguvu anazowekeza kwenye biashara yake na uwezo wake wa kujenga na kuiongoza timu yake.

Kama unajisikia kupata mafanikio.....eleza hilo! Kama unapata pesa na kujenga maisha yako ya baadaye.....sema hivyo! Lakini kila mara weka mkazo kuwa mafanikio ndani ya Green World yanategemea uzoefu binafsi, uwajibikaji wa mwanachama, na kukua kwa mwanachama kibiashara. Shuhuda mzuri kuliko mwingine ye yote wa mafanikio ya biashara ya Green World, ni mtu aliyeshiriki. Kwa hiyo, wape watu taarifa kuhusu fursa hii ya biashara, wape dondoo za nguvu ya mpango wa malipo wa kampuni hii kisha waalike kushiriki katika biashara hii.

Kikubwa zaidi ya maelezo ya pesa unayopata na mafanikio yako uliyoyafikia, kwao ni kiasi watakachopata. Ni muhimu kuwasisitizia kuwa pamoja na kwamba fursa ya Green World ndiyo fursa bora, ni juhumu lao kuchagua na kuendesha biashara wanazozitaka. Green World itawapa msaada mkubwa...... lakini mafanikio ya kila mmoja wao itategemea juhudi zake. Watu watapenda kiasi cha pesa unazozipata, lakini hawataweza kuzitumia! Msaidie kila mmoja kufikia mafanikio yake.

Kusajili Wanachama

Kutokana na presentations ambazo utaendelea kuzitoa, baadhi ya watu watavutiwa si na bidhaa za Green World tu, bali na fursa ya biashara ya mtandao ya kampuni hii. Unapomsajili mwanachama, unamfundisha ili awe mfanya biashara ndani ya timu. Kwa njia hiyo utajenga na kukuza jumuia yako ya wafanyabiashara. Ni kazi yako kufundisha na kutoa maelekezo baada ya kusajili. Kumbuka kuwa mtaalamu ni mtu ambaye kla siku anaendelea kujifunza. Watu uliowasajili watafuata mfano wako wa kutumia njia za kitaalamu.

Kupima Matokeo

Inafaa kupata muda wa kutulia na kufanya tathmini ya mafanikio yako. Kama kuna kitu kilichukua muda mrefu zaidi kukikamilisha kuliko ilivyotegemewa, badili mfumo wako kiutendaji na wataarifu wana jumuia yako kuhusu ugunduzi wako ili kuwaponya kutoka kwenye janga la kupoteza muda mwingi kabla ya kukifanikisha kitu hicho.

Kadri unavyojitathmini, utagundua kuwa kuna mambo uliyafanya vizuri sana. Usisite kujipongeza kwa kufanya vizuri.





<<<< MWANZO